Vita mpya kwa Simba SC na Yanga SC ni namna zinavyopambana kuonyeshana jeuri ya fedha, kumshawishi kiungo wa Azam, Feisal Salum 'Fei Toto', zikimtengea mamilioni ya kufuru kwa ofa tofauti lakini pia ipo klabu moja ya Sauzi.
Licha ya masharti mazito yaliyopo kwenye mkataba wa Fei Toto, wakubwa hao kila mmoja anapambana akiwa na hesabu zake tofauti kichwani.
Yanga SC wanafikiria kumuuza staa wao Aziz Ki kwa Waarabu mwisho wa msimu na mkwanja wote watauelekeza kumalizana na Azam FC na staa huyo ili arejee Jangwani.
Lakini Simba SC nao kocha Fadlu Davids hesabu zake na viongozi zipo kwa Fei ambapo za ndani kabisa zinasema kwamba Simba SC wako hatua za mwisho za kuanza mchakato huo na watawapa Azam SC mkwanja pamoja na wachezaji wawili wazawa ili kumnasa staa huyo.
Credit × Mwanaspoti