Web

Wahofiwa Kufa Maji Ziwa Victoria

Wahofiwa Kufa Maji Ziwa Victoria


TAKRIBAN watu saba wanahofiwa kufa maji, baada ya boti ya mizigo waliyokuwa wakisafiria kutoka kisiwa cha Kalangala, nchini Uganda, kupigwa na upepo mkali na kupinduka kwenye Ziwa Victoria.

Watu watano waliokolewa na mashua ya wavuvi.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani mkasa huo ulitokea alfajiri ya Jumatatu, saa 3:00 asubuhi.

Boti hiyo ilikuwa imebeba mkaa kutoka kisiwa cha Kalangala hadi jiji la Entebbe lililo kando ya ziwa kubwa zaidi la maji safi barani Afrika.

Mmoja wa walionusurika, Moses Bukenya, alisema walikuwa watu kumi na wawili ndani ya boti hiyo iliyoharibika.

"Kabla ya mashua kupinduka, coxswain alituambia kwamba maji yalikuwa yakijaa kwenye boti, na tukaanza kurusha mifuko ya mkaa baharini. Hata hivyo, mashua hatimaye ilipinduka, manusura walio hai waking'ang'ania magunia ya mkaa," alisimulia katika mahojiano na Gazeti la eneo hilo, New Vision.

Katika miaka ya hivi karibuni, usafiri wa majini nchini Uganda umekumbwa na majanga.

Mwaka 2023, takriban watu 20 walikufa, baada ya boti ya abiria iliyojaa kupita kiasi kupinduka katika Ziwa Victoria. 

Vile vile mwaka 2018 Novemba, boti lilipinduka na kuua abiria 30 katika Ziwa Viktoria.


BBC

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad