Web

Wanaompinga Tundu Lissu, Wadai Kauli zake zinawanyima Uhuru wa Kutoa Maoni



Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje chadema John Mrema amesema kauli ya Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu, akihutubia mkoani Iringa kuwa, "wote wanaoona, No Reforms, No Elections haiwezekani ni wana-CCM pamoja na vibaraka wao" ni kauli ambayo inazuia wao kuwa huru kutoa maoni.

Pia amegusia kauli iliyotolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kamati ya hicho ya kuchangisha fedha, Godbless Lema kuwa "wote wanaotaka ubunge au udiwani bila reforms waondoke CHADEMA", sio kauli nzuri kwani inafukuza watu wenye maoni mbadala ndani ya chama chao.


Aidha Mrema amezungumzia kauli kadhaa zilizotolewa na Maria Sarungi hivi karibuni

“Hivi karibuni, Mwanaharakati, Maria Sarungi, aliandika katika ukurasa wake wa “X” akikitaka Chama kiyaweke hadharani majina ya wote wanaotaka ubunge kwa udi na ubani bila reforms, na akatuhumu kuwa watu hao wanataka kufanya “blackmail” (kutishia) eti watahama chama. Pia, Maria Sarungi, bila kujali mamlaka ya Ofisi yako, ametaka ajulishwe ni nani amewaita watiania kwenye mkutano huo maalum maana uongozi mzima upo field. Na akataka Chama kisiwahusishe watiania (“do not engage them”), bali waachwe waende CCM. Kauli hizi za Maria Sarungi (ambaye si mwanaChadema), zinafanana na kauli za Mhe. Lissu na Mhe. Lema. Aidha, kauli hizi zinaingilia mamlaka ya ndani ya Chama, na Ofisi yako imezinyamazia kimya, huku kukiwa na taarifa kuwa Mwanaharakati huyo ana mgongano wa kimaslahi wa kutaka Chama kisishiriki uchaguzi wa mwaka huu kwa maslahi yake binafsi. Kauli za Maria ambaye ni swahiba wa karibu wa baadhi ya viongozi wetu wakuu zinazidi kuongeza vitisho na kufinya uhuru wa maoni kuelekea katika kikao maalum”- Mrema.


John Mrema, mmoja wa wanaounda kundi la G-55 ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisoma waraka wao kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA wakati akizungumza na wanahabari kwa niaba ya wenzake ambao baadhi walikuwapo eneo hilo mkoani Dar es Salaam siku ya Jumapili Aprili 6, 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad