Web

Yanga Yamjibu Kibabe Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Hii Vita ni Kubwa




Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiku kutoa ahadi ya kiasi cha Tsh milioni 60 kwa kikosi cha Tabora United ikiwa kitaibuka na ushindi dhidi ya Yanga SC, klabu ya Yanga imejibu mapigo.

Yanga SC wamejibu mapigo kwa kufanya hamasa kubwa Mkoani Tabora kuelekea katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Jumatano katika Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.

Mkurugenzi wa Wanachama wa timu hiyo Ibrahim Samuel (@i_sammjr ) na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa kikosi hicho Ali Kamwe wameongoza hamasa ya kuendesha Baiskeli na kula chakula cha mchana na mashabiki wa timu hiyo katika uwanja wa Chipukizi.

Ikumbukwe mchezo wa kwanza wa timu hizo uliochezwa Jijini Dar es Salaam ulimalizika kwa Yanga SC kufungwa mabao 3-1.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad