KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mohamed Bajaber amesimulia namna alivyokuwa anapitia wakati mgumu kipindi alipokuwa anasumbuliwa na majeraha na ilibaki kidogo aondolewe kikosini bila kuonja mechi ya mashindano.
“Ni kipindi kigumu kwa mchezaji kukaa nje bila kucheza, inahitaji moyo wa uvumilivu na kutokukaa tamaa, nilikuwa naumia moyo sana kuona wenzangu wanacheża halafu mimi nauguza majeraha kwa muda mrefu, sina maana kwamba sipendi wacheze wengine ila nilitamani kuona natoa mchango wangu,”
“Baada ya kurejea katika ufiti kabla ya kuondoka kwa kocha Dimitar Pantev alitaka kuniondoa jambo ambalo lilikuwa linaniumiza kwani Simba ni klabu kubwa inayojenga CV ya mchezaji, hivyo kingekuwa kitu kibaya kwangu.”
“Angalau jina langu litatajwa kwa kucheza mechi, ilikuwa inaniumiza kuona lingeishia kutajwa katika usajili lakini nisicheze.”

