Kengold vs Simba.
Kinainuliwa kibao dk ya 64, Kengold wanataka kufanya ‘Sub’ Benard Morrison atoke nje. Mwamba anagoma. Baada ya dakika kadhaa, kocha anajaribu tena kumtoa Morrison nje, anagoma tena😂
Baada ya mechi Morrison anaulizwa kwanini uligoma, na haya ndio yalikua majibu yake;
“Hii mechi kwangu ilikua ni mazoezi. Na mimi mazoezi yangu ni lisaa limoja na nusu ( Dakika 90), kwahiyo siwezi kuacha mazoezi labda ndani ya dakika 50 au 60 halafu nitoke nje, haiwezekani.”
Mwamba akaendelea kusema..
“Mwalimu anaona kuna wachezaji wengi wanapoteza mipira mara nyingi, sasa unawaacha ndani, halafu unataka kumtoa Benard Morrison ambae nimecheza vizuri, ah jamani haiwezekani”
Toto tundu, Benard Morrison akielezea kwanini kwa ‘Busara zake’ aliona asitoke uwanjani japokua kocha alifanya sub mara mbili ili atoke nje
Vipi watu wa boli, Je morrison ana hoja? 😀
Alikataa kuolewa ili amkomboe mama yake... Lakini mama ndiye aliyemuuza!
GORYANAH –Hii ni story ya Moto Sana yenye hisia na Mafunzo, binti jasiri anayepambana na siri nzito, umaskini na hatari kubwa kwa ndoto zake! Pakua app yetu ufurahie Sehemu ya 1 Hadi ya 5,na mwendelezo wake kila JUMAMOSI SAA MOJA KAMILI JIONI BURE!
Ukiona ujumbe wa allow notification bonyeza allow ili uwe mwanafamilia.