50 Cent Amtaja Diddy kuwa Adui yake Anayempenda

Rapa, producer na muigizaji wa Marekani 50 Cent amemtaja Diddy ni Adui/Mhalifu wake anayempenda zaidi.

50 Cent ameongea hilo kwenye Interview aliyofanya baada ya kuulizwa kuhusu shujaa wake na mhalifu anayemkubali ambapo amemtaja Diddy.

Tayari 50 Cent ameachia Documentary ya ‘Sean Combs: The Reckoning’ inayohusu maisha ya Diddy, kufeli kwake, matukio yaliyomtokea na kesi zilizompeleka gerezani.

Zaidi ya miaka sasa 50 Cent na Diddy hawapikiki chungu kimoja,hawana uhusiano mzuri, chuki na utani wa kudhalilishana hadharani kati yao.

Related Posts