Shabiki wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Michel Kuka Mboladinga maarufu Lumumba, amezawadiwa gari aina ya Jeep na Rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi, kwa kuitangaza nchi hiyo kwenye michuano ya AFCON 2025.
Lumumba alikuwa akisimama na kunyanyua mkono juu muda wote wa michezo ya timu hiyo, akiiga sanamu maarufu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Patrice Lumumba.
