Diamond Platnumz Alitumia zaidi ya Milioni 200 Kumtibu Mkubwa Fella

Don Fumbwe amedai kuwa, ukiachana na gharama za matibabu ya Mkubwa Fella hapa Tanzania na India zilizogharimu zaidi ya Tsh milioni 200, Diamond alimpa mke wa Mkubwa Fella dola 20,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 50 za Kitanzania kama pesa ya ziada nje ya matibabu. Baada ya kurejea, alipeleka milioni 20 mara mbili na milioni 15 mara moja, jumla ya Tsh milioni 55, katika nyakati tofauti.

Amesema pesa hizo zilikuwa kwa ajili ya matibabu madogo madogo na kliniki baada ya matibabu makubwa ya India.

“Familia ikaanza kulalamika kuwa Diamond anazuia watu wengine kutoa msaada. Diamond akajisikia vibaya ili watu wengine wapate nafasi, kwa sababu tayari alikuwa ameshafanya mambo makubwa ya kimatibabu.” Amesema -Donfumbwe

Related Posts