Sabrina Fella Amchana Don Fumbwe “Alikuwa Boda Boda Kabla Mkubwa Fella Hajakupeka Kwa Mondi”

Baada ya jana Mhasibu wa Diamond Platnumz, Don Fumbwe, kufanya mahojiano na kudai kuwa Diamond tayari ametumia zaidi ya milioni 200 kumtibu meneja wake Mkubwa Fella, mtoto wa Fella, Sabrina Fella, amejitokeza na kupinga vikali madai hayo. Amedai kuwa Fumbwe anaeneza maneno ya uongo na kumtaka aache “uchawa”, akisisitiza kuwa Diamond hajawahi kutoa kiasi hicho cha fedha.

Aidha, Sabrina amemkumbusha Fumbwe kuwa nafasi aliyonayo sasa ni matokeo ya msaada mkubwa aliopata kutoka kwa baba yake, Mkubwa Fella, kwani hapo awali alikuwa dereva bodaboda kabla ya Fella kumkutanisha na Diamond.

Kwa mtazamo wangu, malumbano haya ya mitandaoni hayana tija. Ni jambo la kusikitisha kuona watu wa familia waliowahi kufanya kazi pamoja kwa zaidi ya miaka 10 wakitupiana maneno na kudhalilishana hadharani.

Cha msingi kwa sasa ni kuhakikisha Mkubwa Fella anapatiwa matibabu sahihi na anapona. Masuala mengine yaachwe pembeni. Ni busara kwa watu wote waliopo kwenye pande hizi mbili kuwa watulivu, waache kutupiana lawama na kuepuka mivutano isiyo ya lazima mitandaoni.

Hopetyga

Related Posts