
Tume ya uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Kaguta Museveni kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Alhamisi wiki hii, akiwa na jumla ya kura 7,946,772 ambayo ni asilimia 71.65% ya kura zote zilozopigwa.
Mpinzani wake wa karibu Robert Ssentamu Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine alikuwa wa pili, akiwa na jumla ya kura 2,741,238 au asilimia 24.72%.
Kwa mujibu wa tume hiyo, kura 11,366,201 zilipigwa katika uchaguzi huu wa mwaka 2026, ikiashiria asilimia 52.50% ya idadi ya wapiga kura waliojitokeza kushiriki.
Hata hivyo, kura 275,353 (2.42%) zilizopigwa zilikuwa batili.
Matokeo ya uchaguzi
Museveni 7,946,772 (71.65%)
Bobi Wine 2,741,238 (24.72%)
Bulira Frank 45,959 (0.41%)
