Cairo/Algiers YouTuber maarufu duniani, iShowSpeed, amefichua ukweli wa kilichotokea nyuma ya pazia kuhusu IRL stream yake ya Cairo nchini Misri, na sababu iliyosababisha video hiyo kuondolewa, wakati akizungumza kwenye stream yake ya Sahara akiwa Algeria.
Speed alisema kuwa kuelekea mwisho wa stream yake ya Misri, alikodi boti binafsi na kabla ya kuanza safari aliuliza kama muziki uliokuwa ukichezwa ungeleta matatizo ya copyright. Alithibitishiwa kuwa hakungekuwa na shida yoyote, ndipo akaendelea na stream kama ilivyopangwa.
Hata hivyo, baada ya stream kumalizika, Speed alishtushwa kugundua kuwa msanii mmoja wa Misri alikuwa ame-claim VOD nzima ya stream kupitia copyright, akilenga kuchukua mapato yote ya matangazo (ad revenue) ya video hiyo.
Kile ambacho msanii huyo hakukijua ni kwamba YouTube inaruhusu creator kuondoa au kubadilisha sehemu zenye copyright. Speed alichukua hatua haraka kwa kuondoa sauti iliyodaiwa, akaibadilisha na muziki wa bure wa YouTube (copyright-free), kisha aka-upload upya video hiyo.
Kutokana na hatua hiyo, dakika za mwisho za stream ya Cairo sasa zinaonekana zikiwa na muziki wa kawaida wa stock, huku sauti halisi ya Speed ikiwa imezimwa, baada ya jaribio la kuchukua mapato ya stream hiyo kushindikana.
Tukio hili limeibua mjadala mkubwa mtandaoni kuhusu copyright, matumizi ya muziki kwenye live streams, na changamoto wanazokutana nazo creators wanaposafiri na kufanya maudhui katika nchi tofauti.
