Mlinda lango wa zamani wa klabu ya Singida Black Stars na timu ya Taifa ya Tanzania Hussein Masalanga ametambulishwa na klabu ya Yanga kuwa nyota mpya wa klabu hiyo.
Masalanga aliisaidia Taifa Stars kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza na kuandika historia ya kuwa golikipa wa kwanza kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON akiwa na Taifa Stars.
