Fahyvanny Aikana DM ya Kumuomba Msamaha Paula

Mwanamitindo Fahyvanny (Fahyma) ameibuka vikali mtandaoni kukanusha madai ya uongo yaliyoenea yakidai alimuomba msamaha Paula. Kupitia Instagram, Fahyvanny aliweka wazi screenshot ya DM hiyo na kuwasilisha ujumbe wa kejeli, akisisitiza hajawahi kumuomba mtu yeyote msamaha tangu azaliwe.

Akiwalenga waliotengeneza picha hizo feki, Fahyvanny aliandika, “Mnikomeeeee… acheni mara moja,” akionyesha kuchoshwa na propaganda za mitandaoni. Picha iliyosambaa ilidai kumuonyesha akijinyenyekeza na kuomba radhi kwa Paula kutokana na maneno ya nyuma madai aliyoyakana moja kwa moja.

Mvutano kati ya Fahyvanny na Paula Kajala unatokana na historia ya mahusiano yao na msanii Rayvanny, suala ambalo limekuwa likitikisa mitandao kwa miaka. Kauli ya Fahyvanny sasa inaweka wazi kuwa hakuna mazingira ya kati yao, na amewataka watu wakubali hali ilivyo bila kubuni simulizi za uongo

Related Posts