Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limezindua rasmi ratiba ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 katika Mashindano ambayo yatafanyikia Afrika Mashariki.
Kulingana na CAF, kampeni ya kufuzu itafanyika 2026, ikianza na duru ya awali iliyopangwa Machi.
CAF ilitangaza pia kuwa mechi za hatua ya makundi za kufuzu kwa AFCON 2027 zitachezwa katika madirisha matatu ya Kimataifa mwishoni mwa 2026.
Mechi za 1 na 2 zimepangwa kufanyika Septemba 21 hadi 30, 2026, zikifuatwa na siku za Mechi 3 na 4 kuanzia Oktoba 1 hadi 6, 2026.
Raundi ya mwisho ya ratiba ya makundi, siku za Mechi 5 na 6, itakuwa kati ya Novemba 9 na 17, 2026.
Michuano hiyo ya kufuzu ndiyo itakayoamua timu zitakazojihakikishia nafasi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika 2027, ambazo CAF imethibitisha kuwa zitaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Tanzania na Uganda.
