Huruma, Yanga Yapokea Kichapo Kitakatifu Kutoka kwa Al Ahly

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamekubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa leo Januari 23, 2026, kwenye Uwanja wa Borg El Arab, nchini Misri.


Dakika ya 45+3, zikiwa zimesalia sekunde chache kabla ya timu kwenda mapumziko, nyota wa Al Ahly, Mahmoud Trezeguet, alifunga bao la kwanza na kuwapa wenyeji uongozi.
Kipindi cha pili, dakika ya 75, Trezeguet aliongeza bao la pili ambalo lilibaki mpaka mwisho wa mchezo, na kuipa Al Ahly ushindi dhidi ya wapinzani wao.


Kufuatia matokeo hayo, Al Ahly wanaongoza Kundi B wakiwa na pointi 7, wakifuatiwa na Yanga SC wenye pointi 4 baada ya kucheza michezo mitatu.


Timu za AS FAR na Kabylie zina pointi 1 kila moja, zikiwa zimecheza michezo miwili.

Related Posts