Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, katika kikao chake kilichofanyika leo January 25, 2026 Zanzibar, imepitia na kujadili kisha kufanya uteuzi wa
Wagombea uongozi wa CCM wanaotokana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo upande Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wanaotokana na Bunge kutoka upande wa Tanzania Bara (Nafasi 3) Wanaume walioteuliwa kugombea (nafasi 2) ni Paul Makonda na Livingstone Lusinde na kwa upande wa Wanawake (nafasi 1) ni Asia Halamga.
Kwa upande wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wanaotokana na Bunge kutoka upande wa Zanzibar (nafasi 2) walioteuliwa ni Wanaume (nafasi (1) Khamis Mussa Omar na Wanawake (nafasi 1) Tauhida Cassian GALOS.
Katibu wa Wabunge wote wa CCM (nafasi 1), Agnes Elias Hokororo, Wenyeviti wa Bunge (nafasi 3) ,Najma Murtaza Giga, Deodatus Philipo Mwanyika na Cecilia Pareso.
