Ahmedy Ally; Tunaenda Ishangaza Africa Simba Inaingia  Robo Fainali CAF

Nimetua Dar Es Salaam nikitokea Tunisia Baada ya kushusha mguu na kuliona Jiji la Dar Es Salaam, Kisha nikavuta hewa ya Joto la Salaam , Halafu nikawaona baadhi ya mashabiki wa Simba Uwanja wa Ndege, nikapata matumaini mapya ya timu yetu kufanya kufuru katika mechi tatu za mwisho za Makundi

Jumapili ya Feb 01 Tunaanza kuandika Historia itakayotikisa na kuishangaza Afrika, Sisi kwetu bado tunaiona Robo Fainali tena sio kwenye ndoto bali kwenye mipango

Wana Simba nawaomba mtuunge mkono kwenye kufanikisha azma ya kuitafuta Robo Fainali ya nane mfululizo Hakuna kuishiwa Pawa kila Mwana Simba abebe matumaini haya twende kwenye mapamba”Ameandika-Ahmed Ally

Related Posts