Klabu ya Simba imemtambulisha Anicet Oura nyota raia wa Ivory Coast baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili juu ya nyota huyo aliyewahi kukipiga Asec Mimosas pamoja na Stellenbosch ya Afrika Kusini.
Oura anamudu kucheza kama winga pamoja na namba 10 na amekuja kuongeza nguvu katika eneo la Ushambuliaji la klabu ya Simba.
