Bilionea Bill Gates amekanusha vikali madai yanayodai kulikuwa na jitihada za kuficha maambukizi ya ugonjwa wa zinaa (STD), huku akisema anajutia kila dakika aliyowahi kutumia na mfadhili aliyefariki, Jeffrey
Kauli hiyo ya Gates imekuja baada ya file jipya la Epstein kudai kwamba Gates alipanga kwa siri kumpa aliyekuwa mke wake, Melinda Gates, dawa za antibiotics baada ya kudaiwa kuambukizwa ugonjwa wa zinaa kutoka kwa wanawake waliotajwa kuwa “Warusi”.
Gates amesisitiza kuwa madai hayo si ya kweli na hayana msingi wa ukweli, akiongeza kuwa uhusiano wake wowote wa awali na Epstein ulikuwa kosa kubwa
Kauli hii pia inajiri baada ya Melinda Gates, aliyekuwa mke wake, kusema kuwa Bill Gates anapaswa kujibu maswali kuhusu taarifa na madai yaliyomo katika mafaili ya Epstein ambayo yamekuwa yakizua mjadala mkubwa duniani.
Hadi sasa, hakuna uthibitisho rasmi uliotolewa na mamlaka kuthibitisha madai hayo yaliyomo kwenye barua pepe hizo, huku mjadala wa umma ukiendelea kufuatia kufunguliwa kwa nyaraka zaidi zinazohusiana na kesi ya Epstein.
