Makamu wa Rais Aongoza Mazishi ya Mbunge Munde Tambwe Tabora

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Munde Tambwe, yaliyofanyika Februari 4, 2026, nyumbani kwao Kata ya Cheyo, Manispaa ya Tabora. Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi wa Serikali, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wabunge, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wananchi waliokuja kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.

Munde Tambwe alifariki dunia Februari 2, 2026, jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Baada ya taratibu za kitaifa na kifamilia kukamilika, mwili wake ulisafirishwa hadi mkoani Tabora na kuzikwa katika makaburi ya Sheikh Yahaya yaliyopo Kata ya Kidongo Chekundu.Kusoma Zaidi, Bonyza hapa.

Related Posts