Waziri Rajabu Ateuliwa na Rais Samia Kuwa Katibu Mkuu Viwanda na Biashara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Waziri Rajabu Salum kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Kurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka imesema uteuzi huo umefanyika leo Februari 6, 2026.

Balozi Waziri anachukua nafasi ya Dkt. Hashil Twaib Abdallah ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Aidha uapisho wa Balozi Waziri na viongozi wengine unatarajiwa kufanyika siku ambayo utapangiwa.

Related Posts