Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu inaendelea tena leo, Jumatatu Februari 09.2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam
Kesi hiyo No. 19605/2025 inayosikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, imepangwa kusikilizwa kwa muda wa siku 20 mfululizo kuanzia leo hadi Machi 06.2026
Ikumbukwe kuwa, kesi hiyo kwa sasa ipo kwenye hatua ya mashahidi wa Jamhuri kuendelea kutoa ushahidi wao Mahakamani hapo, hata hivyo mara ya mwisho kutajwa Mahakamani hapo mshtakiwa (Tundu Lissu) ambaye anajitetea mwenyewe aliwasilisha mapingamizi kadhaa ambayo bila shaka leo upande wa Jamhuri wataanza kwa kuyajibu mapingamizi hayo.
