Kidoa Aibua Taharuki Mitandaoni, Picha Tata na Kauli Yake Yazua Mjadala Mkubwa

MSANII wa filamu za Kibongo na aliyewahi kujizolea umaarufu mkubwa kama muuza sura kwenye video mbalimbali za muziki, Asha Salum maarufu kama ‘Kidoa’ , ameibua gumzo jipya mitandaoni baada ya kuanza kuonyesha mabadiliko makubwa ya maisha yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kwa siku za hivi karibuni, Kidoa amekuwa akichapisha picha na video zinazoonyesha maisha ya kujiachia na starehe, huku baadhi ya maudhui hayo yakitajwa na mashabiki kuwa ya “tata” na yanayoibua mjadala mkubwa.

Muonekano wake mpya pamoja na aina ya post anazoweka zimeanza kuwashangaza wengi, hasa wale waliomzoea kama msanii mtulivu na mwenye taswira tofauti na anayoionyesha sasa.

Mbali na picha hizo, Kidoa pia ameonekana akifurahia maisha ya mapumziko katika maeneo mbalimbali ya kitalii, ikiwemo Zanzibar, ambako amekuwa akishiriki matukio, matembezi ya fukweni na kujionyesha akiwa katika hali ya furaha bila kujali maneno ya wakosoaji.

Hatua hiyo imeonekana kama ishara ya kujiamini na kuamua kuishi maisha yake kwa masharti yake mwenyewe.

Wakati mijadala ikiendelea kushika kasi, Kidoa aliongeza mafuta kwenye moto baada ya kuandika ujumbe wenye utata kupitia Instagram, akisema:

“Kama dhambi zako hazikupe pesa basi hayo ni matumizi mabaya ya dhambi.”
Kauli hiyo ilisambaa kwa kasi na kuzua tafsiri tofauti miongoni mwa watumiaji wa mitandao.

Wapo walioichukulia kama utani au falsafa ya maisha ya kujitegemea, huku wengine wakiona kama kauli inayoweza kuhamasisha maadili yasiyofaa kwa jamii.

Related Posts