
Kimenuka kwa majirani +254!
Mwanaume anayetajwa kuwa raia wa Urusi, Yaytseslav anatrend kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa video kibao alizowarekodi wanawake nchini Kenya.
Katika video hizo zinazodaiwa kuwa zilirekodiwa kwa miwani maalum aliyokuwa ameivaa, jamaa anaonekana ‘akiwatokea’ wanawake tofautitofauti katika maeneo ya umma jijini Nairobi na kuwashawishi kwenda naye kwenye nyumba aliyofikia.
Ajabu ni kwamba, karibu asilimia 99 ya wanawake aliowarekodi, walikubali kuondoka naye na baadaye wanaonekana wakiwa chumbani.
Katika video hizo, mwanaume huyo huonekana kuanza mazungumzo mepesi kisha kuwashawishi wanawake hao kuondoka naye, hali iliyowashangaza wengi kufuatia urahisi wa mbinu aliyokuwa akiitumia.
Vipande vifupi vya matukio hayo vimesambazwa katika mitandao ya kijamii ikiwemo TikTok na YouTube, huku taarifa zikidai kuwa video ndefu zenye maudhui ya faragha zaidi huuzwa kupitia chaneli binafsi ya Telegram.
Hali hiyo imeibua taharuki nchini Kenya, wengi wakimtuhumu kwa kuwalaghai wanawake kisha kuwarekodi kwa lengo la kujipatia umaarufu na fedha mitandaoni.
Mjadala mkubwa umeibuka kuhusu ridhaa na faragha, huku wakosoaji wakisisitiza kuwa kukubali kuonana na mtu hakumaanishi kutoa ruhusa ya kurekodiwa au kusambaziwa video mtandaoni.
Watoa maoni mbalimbali wamekosoa vikali vitendo hivyo, wakivitaja kuwa ni uvamizi wa faragha na ukiukwaji wa haki na heshima za msingi za binadamu.
Yapi maoni yako? Mrusi amezingua au wanawake waliokuwa wakimkubali kirahisi ndiyo wamezingua?
