
Asiye na wake aelekee jiwe. Jane Leperet Maiyan alikuwa amekata tamaa kabisa kwamba Josephat Ole Meripet atakuwa wake. Akipatana naye anamsalimia kwa heshima, anarembua macho, anacheka cheka na kumguza guza mabega ilimradi ajionee kuwa amemteka mawazo. Lakini wapi. Josephat hakupania kuyaona hayo.
Jane akashikwa na hamaki na hatimaye akamuitisha nambari ya simu. Akawa anamtumia jumbe fupi fupi za utani Whatsapp, huku akimuuliza tumaswali twa kumsoma kama ana hisia za kimapenzi kwake. Puuuuu…SOMA ZAIDI
