
Shirikisho la soka la Senegal (FSF) limeapa kupinga uamuzi wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) ulioipa Morocco Ubingwa wa mezani wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, na kuthibitisha mipango ya kupeleka masuala hayo katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo ya FIFA (CAS).
Katika uamuzi wa kihistoria, bodi ya rufaa ya CAF iliamua kwamba timu ya taifa ya Senegal ilipoteza fainali ya AFCON baada ya wachezaji kadhaa kutoka uwanjani hadi kwenye chumba chao cha kubadilishia nguo wakipinga uamuzi wa Mwamuzi.
Uamuzi huo ulisema Senegal ilikiuka vifungu vya 82 na 84 vya kanuni za AFCON walipotoka uwanjani wakati wa mchezo.
Itakumbukwa kuwa takribani mashabiki 18 wamefungwa nchini Morocco baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika vurugu wakati wa fainali hiyo iliyofanyikia nchini Morocco.
