
Bao la dakika za lala mkono wa Buriani kutoka kwa Ismael Mhesa linaharibu sherehe ya Eid AL-FITRI kwa Wananchi, Young Africans kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Wakata Miwa, Mtibwa Sugar FC katika dimba la Jamhuri Dodoma.
Kwa sare hiyo ya tatu mfulululizo kwa Wananchi, linaibakisha Yanga SC kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania bara alama 38 baada ya mechi 16.
FT: Mtibwa Sugar FC 1-1 Yanga SC
90+1’ Ismael Mhesa
23’ Pacome Zouzoua.
