Kiongozi Mkuu wa IRAN Afunguka “Hongereni Wananchi Mmelinda Iran”

Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei, ametoa pongezi kwa Wananchi wa Iran kufuatia kusitishwa kwa muda wa wiki mbili kwa vita kati ya Iran dhidi ya Israel na Marekani iliyoanza tangu Februari 28 2026.

Khamenei ameelekeza pongezi zake kwa Wananchi wa Iran akisisitiza kuwa wao ndio waliobeba jukumu kubwa la kuilinda Nchi na kuwa mshikamano na uthabiti wao ndiyo vimeifanya Iran kuendelea kusimama imara katika kipindi chote cha mapigano “hongera kwa ushindi huu kwa Taifa la Iran na wapenda uhuru wote Duniani, ni ninyi Wananchi mlioiongoza Nchi”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Vyombo vya Habari vya Iran, makubaliano ya kusitisha vita yanatarajiwa kujadiliwa Mjini Islamabaad Nchini Pakistan kuanzia April 10, 2026 ambapo Iran imeipa Marekani masharti kumi kabla ya kusitisha vita

Related Posts