
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kupitia mitandao ya kijamii na mchambuzi wa Crown FM, Hans Raphael, Taarifa hizo zinazohusiana na mchezaji Selemani Mwalimu kuelekea dirisha la usajili la mwisho wa msimu.
Rais wa Heshima wa Simba Mohamed Dewji ameingilia kati suala la mshambuliaji wa Simba Suleiman Mwalimu ambaye yuko kwa mkopo akitokea Wydad Casablnca ili kuangalia uwezekano wa kumsajili moja kwa moja au kuongeza mkataba wa mkopo, Hii ni baada ya Taarifa zimeeleza kuwa klabu ya Yanga imefungua mazungumzo na Wydad Casablanca kuhusu uwezekano wa kumsajili mshambuliaji Selemani Mwalimu kwa mfumo wa mkopo kuelekea dirisha kubwa la usajili la mwisho wa msimu huu. Mazungumzo hayo yameripotiwa kuhusisha makubaliano ya awali ya kifedha pamoja na masharti ya uhamisho wa muda.
Imeelezwa kuwa Yanga iko tayari kutoa kiasi cha dola za Marekani 50,000 kama ada ya mkopo katika mpango unaojadiliwa kati ya pande husika. Kiasi hicho kimeelezwa kuwa sehemu ya jitihada za klabu hiyo kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa msimu ujao, ambapo inatafuta kuongeza nguvu ya kikosi chake kwa mchezaji mwenye uzoefu wa ushindani wa kimataifa na ligi ya ndani.
Selemani Mwalimu kwa sasa anahusishwa na uhamisho wa mkopo uliopo kati ya Wydad Casablanca na Simba, ambapo mkataba wake wa muda unatarajiwa kufikia mwisho wake mwishoni mwa msimu huu. Hali hiyo imefungua nafasi ya klabu mbalimbali kuingia kwenye mazungumzo ya awali ya kumsajili mchezaji huyo baada ya kipindi chake cha mkopo kukamilika.
Katika taarifa hizo imeelezwa kuwa Yanga inamuona Mwalimu kama mchezaji mwenye uwezo wa kuongeza ushindani katika safu ya mbele na kuleta mabadiliko ya kiufundi ndani ya kikosi. Mazungumzo kati ya pande zinazohusika yameripotiwa kuwa katika hatua za awali huku maamuzi ya mwisho yakisubiri kukamilika kwa taratibu za uhamisho na makubaliano ya kimkataba.
Taarifa zinaongeza kuwa mchakato huo unahusishwa moja kwa moja na mipango ya maandalizi ya dirisha la usajili, ambapo klabu mbalimbali huanza kufanya tathmini ya wachezaji waliopo kwenye mikopo au wanaokaribia kumaliza mikataba yao ya muda. Hali hii imefanya jina la Selemani Mwalimu kuibuka katika mjadala wa usajili kutokana na nafasi yake ya sasa ya kimkataba.
Kwa upande wa Simba, mchezaji huyo yuko katika kipindi cha mwisho cha mkopo wake, ambapo atarejea kwenye uamuzi wa mkataba wake wa msingi baada ya msimu kumalizika. Hali hiyo imeacha nafasi wazi ya klabu nyingine kuingia kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na mmiliki wa mkataba wake, Wydad Casablanca, kuhusu hatma yake ya baadaye.
