Yanga Waachana na Kocha Pedro Gonçalves, Moalin na Mabedi Kuchukua Majukumu

Klabu ya Yanga imetangaza kuachana rasmi na kocha wake mkuu Pedro Gonçalves kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa kwa amani, huku kila upande ukiheshimu mchango wa mwenzake katika kipindi chote cha ushirikiano.

Baada ya kuondoka kwa Gonçalves, majukumu ya kukinoa kikosi cha Wananchi yamekabidhiwa kwa makocha wa muda, Kocha Moalin pamoja na Patrick Mabedi, ambao wataiongoza timu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Hatua hiyo inakuja katika kipindi muhimu cha mashindano, ambapo Yanga wanaendelea kupambania mafanikio katika ligi na michuano mingine.

Mashabiki sasa wanasubiri kuona namna benchi hilo jipya litakavyoiendesha timu katika michezo iliyosalia.

 

Related Posts