Penzi la Harmonize na Kajala Lazidi Kuwavutia Mashabiki Mitandaoni

Penzi la Harmonize na Kajala Lazidi Kuwavutia Mashabiki Mitandaoni
Penzi la Harmonize na Kajala Lazidi Kuwavutia Mashabiki Mitandaoni

Penzi kati ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize na muigizaji Kajala Masanja limeendelea kuzua gumzo kubwa mitandaoni, huku likiwavutia mashabiki wengi wanaofuatilia ukaribu wao.

Wengi wa mashabiki wamekuwa wakionesha kuvutiwa na namna wawili hao wanavyooneshana upendo hadharani, wakisema mahusiano yao yanaonekana kuwa na kiwango kikubwa cha maelewano na furaha.

Baadhi ya mitazamo ya mashabiki imeeleza kuwa kila wanapowaona Harmonize na Kajala pamoja, huhisi kama penzi lao lina mvuto wa kipekee, huku wengine wakidai kuwa mahusiano yao yanaonekana “ya kimataifa” kutokana na namna wanavyooneshana hisia zao.

“I love it when Kajala is with Harmo.. let them be,” aliandika mmoja wa mashabiki.

 

Mwingine aliandika: “Mahusiano yao yanaonekana kimataifa sana,” akionesha kuvutiwa na namna wanavyoishi hadharani, huku wengine wakisisitiza kuwa wawili hao wanaonekana kupendana kwa dhati licha ya changamoto walizowahi kupitia nyuma.

Pia, baadhi ya mashabiki wamewatetea dhidi ya wakosoaji wa mitandaoni, wakisema wanapaswa kuachiwa nafasi yao ya kufurahia maisha yao binafsi bila kuingiliwa.

Historia ya mahusiano ya wawili hao ya kuachana na kurudiana mara kwa mara imeendelea kufanya uhusiano wao kuwa miongoni mwa mada zinazozua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Related Posts