
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC), imemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na mbunge wa zamani wa Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, Aggrey Mwanri kuwa Naibu Katibu Mkuu- Bara akichukua nafasi ya John Mongella.
Uteuzi huo umefanyika leo Jumatano, Julai 29, 2026 katika kikao kilichofanyika Zanzibar chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan na kutangazwa kwa umma na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi.
