
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema nchi ya Tanzania ni salama kuelekea Mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027 ambapo nchi za Tanzania,Uganda na Kenya zinatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Waziri Katambi ametoa kauli huo wakati wa Kikao kilichoongozwa na Waziri Mkuu,Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mashindano ya AFCON.
Waziri Mkuu ameongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar.
