
Baada ya kutambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya Yanga, mshambuliaji wa Kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile ameonesha kufurahishwa na mapokezi aliyopata kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Akimzungumza baada ya utambulisho huo uliorushwa mubashara Azam Sports TV, Shalulile ameeleza kuwa mafanikio hayaletwi na mchezaji mmoja pekee, bali yanajengwa kwa nguvu ya pamoja ya wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki akimaanisha kila kimojawapo tajwa hapo juu kina nafasi muhimu katika kuifikisha Yanga kwenye malengo yake msimu huu.
Peter Shalulile, amesema amekuja kuongeza ubora ndani ya kikosi hicho na anaamini kwa kushirikiana na wenzake watafanikisha makubwa msimu unaokuja na kubainisha kuwa Rais wa Yanga (ambaye yeye alimuita Mwenyekiti), Eng. Hersi Said, amekuwa na mchango mkubwa katika uhamisho wake, akibainisha kuwa kwa muda mrefu alikuwa na ndoto ya kumuona akivaa jezi ya Yanga, jambo ambalo sasa limetimia.
