Sintofahamu Yanga: Depu na Pacome Wakatwa Kikosi cha Msimu Mpya 2026/27 Wiki ya Mwananchi

 

Sintofahamu Yanga: Depu na Pacome Wakatwa Kikosi cha Msimu Mpya 2026/27 Wiki ya Mwananchi
Sintofahamu Yanga: Depu na Pacome Wakatwa Kikosi cha Msimu Mpya 2026/27 Wiki ya Mwananchi

Sintofahamu Yanga: Depu na Pacome Wakatwa Kikosi cha Msimu Mpya 2026/27 Wiki ya Mwananchi

DAR ES SALAAM – Hatma ya mshambuliaji Laurindo Depu na kiungo mchezeshaji Pacome Zouzoua ndani ya Yanga SC imeingia kwenye utata mzito, baada ya majina yao kuachwa nje wakati wa utambulisho rasmi wa kikosi cha msimu wa 2026/27.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na maelfu ya mashabiki katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi kwenye Uwanja wa Uhuru, limezua mjadala mpana kuhusu hatma ya nyota hao wawili.

Akitangaza orodha ya wachezaji watakaovaa jezi za Wananchi msimu huu, Afisa Habari na Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, alitaja safu nzima ya makipa, mabeki, viungo na washambuliaji—lakini jina la Depu halikutoa sauti kabisa. Hatua hii imeashiria wazi kuwa mshambuliaji huyo huenda ameshuka kwenye chati za benchi la ufundi.

Orodha Rasmi ya Wachezaji Kilichotambulishwa:

  • Makipa: Diarra Djigui, Abdultalib Mshery, Hussein Masalanga.

  • Mabeki: Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Shadrack Boka, Ibrahim Bacca, Kouassi Yao, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Erick Mwijage, Denis Nkane.

  • Viungo: Mudathir Yahya, Abdulnassir Abdallah, Mohammed Mussa, Abubakar Nizar, Farouk Komara, Duke Abuya, Allan Okello, Aziz Andambwile, Edmund John, Mohammed Hussein, Aboubakary Salum.

  • Washambuliaji: Max Nzengeli, Fred Ngoma, Peter Shalulile, Ibrahima Touré, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, Clement Mzize, Mohammed Damaro, Issa Abushiri.

Vipi Kuhusu Pacome Zouzoua?

Tofauti na Depu, kukosekana kwa jina la Pacome Zouzoua kunahusishwa moja kwa moja na majeraha ya muda mrefu yanayomsumbula. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa kiungo huyo hatari anaweza kukosa sehemu kubwa au msimu mzima wa 2026/27 akiwa kwenye matibabu na rehabilitation.

Milango ya Kutokea Ipogo?

Wakati Pacome akipambania afya yake, hali ni tofauti kwa Laurindo Depu kwani uongozi wa Yanga haujatoa taarifa yoyote rasmi. Mashabiki wanatamani kufahamu iwapo nyota huyo ataonyeshwa mlango wa kutokea kwa kuvunja mkataba, kutolewa kwa mkopo, au kuuzwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Related Posts