Simanzi Uhuru: Yanga SC Yafungwa na Les Aigles Du Congo Kilele cha Wiki ya Mwananchi

DAR ES SALAAM – Kijana mwenye umri wa miaka 20, Jonny Talasi, amekuwa mwiba mchungu kwa Wananchi baada ya kupiga mabao mawili pekee yaliyowapa ushindi mabingwa wa Kongo, Les Aigles Du Congo, wa mabao 2-1 dhidi ya Young Africans SC kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo huo uliochezwa katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi (Yanga Day), ulianza kwa Yanga kushika usukani mapema kupitia bao la penalti lililowekwa kimiani na mshambuliaji mpya Peter Shalulile mnamo dakika ya 26.

Hata hivyo, furaha ya Wananchi haikudumu kwa muda mrefu kwani Talasi alipindua meza:

  • Daika ya 36: Talasi alisawazisha bao hilo na kufanya ubao usomeke 1-1 kabla ya mapumziko.

  • Dakika ya 65: Mshambuliaji huyo machachari alipachika bao la pili na la ushindi, akiiacha safu ya ulinzi ya Yanga bila majibu.

Matokeo hayo yameiacha klabu ya Yanga SC na maswali kadhaa kuhusu utulivu wa safu yao ya ulinzi kuelekea ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa ligi.

Matokeo ya Mchezo (FT):

Yanga SC 1-2 Les Aigles Du Congo

⚽ 26’ Peter Shalulile (Penalti) — Yanga SC

⚽ 36’ Jonny Talasi — Les Aigles Du Congo

⚽ 65’ Jonny Talasi — Les Aigles Du Congo

Related Posts