
Yanga SC wameendeleza ubabe wao mbele ya Pamba Jiji FC kwa kusepa na pointi tatu
MABINGWA watetezi wa ligi, Yanga SC wameendeleza ubabe wao mbele ya Pamba Jiji FC kwa kusepa na pointi tatu mazima ndani ya uwanja.
Baada ya dakika 90 Agosti 28, 2026 ilikuwa Yanga SC 2-0 Pamba Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex.
Mabao ya Yanga SC yalifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 17 na Ibrahim Toure dakika ya 22 katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Mchezaji bora wa mchezo alichaguliwa kuwa Maxi ambaye amekuwa katika kiwango bora kwenye mechi za mwanzo msimu wa 2026/27.
Unakuwa ni mchezo wa 4, Yanga SC inashinda na Nzengeli anatwaa tuzo yake ya 3 ya mchezaji bora msimu wa 2026/27 alianza kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC akatwaa tuzo hiyo mchezo dhidi ya Coastal Union na mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC.
