RASMI: Erick Mwijage Ndiyo Mbadala wa Aziz Ki Kwenye Dabi ya Kariakoo

RASMI: Erick Mwijage Ndiyo Mbadala wa Aziz Ki Kwenye Dabi ya Kariakoo
RASMI: Erick Mwijage Ndiyo Mbadala wa Aziz Ki Kwenye Dabi ya Kariakoo

RASMI: Erick Mwijage Ndiyo Mbadala wa Aziz Ki Kwenye Dabi ya Kariakoo

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, amethibitisha kuwa Erick Mwijage ndiye atakayejaza nafasi ya Stephane Aziz Ki kwenye Mchezo wa Dabi ya Kariakoo. Kauli hiyo imekuja mara baada ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya St. George.

“Anastahili Kucheza Timu Yoyote Kubwa…”

Mchambuzi wa soka, Privaldinho, ameandika ujumbe mzito kuhusu kipaji cha kijana huyo mdogo:

“Niwe mkweli—nisiposema ukweli huu, hata mawe yatashangaa. Fundi Erick Mwijage alichelewa sana kujiunga na Yanga SC. Angeingia klabuni hapa misimu mitatu iliyopita, hivi sasa tungekuwa tunaongelea mambo makubwa zaidi.

Kwa kipaji chake, anastahili kucheza klabu yoyote kubwa Afrika Mashariki, kuwa na angalau michezo 10 ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na kuwa miongoni mwa wachezaji waandamizi kwenye timu ya taifa.

Lakini hatuwezi kumpangia Mungu majira na nyakati; yeye ndiye mjuzi wa yote. Mwijage mwenyewe aliwahi kusema kuwa kile ambacho wengine wanakiita ‘bahati’, kwake ni ‘baraka za Mungu’. Na bila shaka, haya ndiyo majira yaliyowekwa ili baraka zake zionekane.

Hata hivyo, kipaji bila nidhamu na jitihada ni sawa na pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe. Huu ni wakati wa yeye kuweka jitihada mara tatu zaidi ya awali. Namuombea kila la kheri; Mwenyezi Mungu akamwinue na kumbariki anapomtumainie kwenye kila jambo. Kazi na Sala.

Related Posts