TFF Yaionya Kampuni ya Sandaland Kutotumia Nembo yake

TFF Yaionya Kampuni ya Sandaland Kutotumia Nembo yake
TFF Yaionya Kampuni ya Sandaland Kutotumia Nembo yake

TFF Yaionya Kampuni ya Sandaland Kutotumia Nembo yake

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema limesikitishwa na matumizi ya nembo yake katika mkutano na Waandishi wa Habari ulioandaliwa na Kampuni ya Sandaland Fashion Wear leo Septemba 22, 2026 Jijini Dar es salaam, uliokuwa ukizungumzia suala la jezi za Timu ya Taifa.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Septemba 22, 2026 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, Shirikisho hilo limesisitiza kuwa halikuwa sehemu ya mkutano huo wala halikuwa na taarifa za awali kuhusu maudhui yake.

TFF imeiagiza Sandaland Fashion Wear kuacha kutumia nembo ya Shirikisho hilo katika maudhui ambayo hayahusiani na mkataba uliopo kati ya pande hizo mbili.

Aidha, TFF imesema itaiandikia rasmi kampuni hiyo ili kupata maelezo ya kina kuhusu matumizi ya nembo yake katika mkutano huo.

Related Posts