Nikki wa Pili Ahamiishwa Kutoka Kibaha Kwenda Wilaya ya Songwe

Nikki wa Pili Ahamiishwa Kutoka Kibaha Kwenda Wilaya ya Songwe
Nikki wa Pili Ahamiishwa Kutoka Kibaha Kwenda Wilaya ya Songwe

Nikki wa Pili Ahamiishwa Kutoka Kibaha Kwenda Wilaya ya Songwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na uhamisho wa Viongozi mbalimbali, huku Nickson Simon John, Neema Lugangira, Festo Kiswaga, Stanslaus Shing’oma Mabula na Hassan Omary Bomboko wakiwa miongoni mwa waliopangiwa vituo vya kazi.

Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa leo, Septemba 29, 2026, Neema Lugangira ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Festo Kiswaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, huku Stanslaus Shing’oma Mabula akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya.

Kwa upande wa waliohamishwa, Nickson Simon John (Nikki wa Pili) amehamishwa kutoka Wilaya ya Kibaha kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe, huku Hassan Omary Bomboko akihamishwa kutoka Wilaya ya Hai kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga.

Related Posts