Wakili wa Zamani wa Yanga Arusha Dongo Kwa Kocha wa Yanga Baada ya Kufugwa na Simba

Mwanasheria wa zamani wa klabu ya Yanga, Wakili Simon Patrick ametoa maoni yake kuhusu mwenendo wa klabu hiyo baada ya kupoteza mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba SC akiutaka uongozi wa klabu hiyo kuleta kocha mwenye wasifu mkubwa unaolingana na malengo makubwa ya klabu hiyo.

Wakili Simon amekiri kuwa Yanga SC imefanikiwa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) kuwa na viongozi bora, wachezaji/timu bora, na mashabiki bora lakini amewakosoa viongozi wa klabu hiyo kwa kuendelea kusajili makocha ambao anaona hawana uwezo na wasifu unaolingana na malengo makubwa ya Yanga katika mashindano ya Afrika.

Katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa mitandaoni ya kijamii leo Oktoba 11, 2026, Wakili Simon amemaliza kwa kusema, “Mwalimu wa sekondari hawezi kufundisha Chuo kikuu,” akimaanisha kuwa kocha aliyepo (Manqoba Mngqithi) anaonekana kutokuwa na hadhi au mbinu za kiwango cha juu zinazotakiwa kuivusha Yanga kimataifa.

Related Posts