
Cristiano Ronaldo Afikisha Mabao 981, Abakiza Mabao 19 Pekee Kufikia Record ya Mabao 1,000
RIYADH, SAUDI ARABIA — Mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Al Nassr FC, Cristiano Ronaldo, anaendelea kuandika historia katika ulimwengu wa soka baada ya kufikisha jumla ya mabao 981 katika maisha yake ya soka la ushindani.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 sasa amebakiza mabao 19 pekee ili kutimiza lengo lake kubwa la kihistoria la kufikisha mabao 1,000.
Dondoo za Mchezo: Al Nassr FC vs Neftchi Fargona
Ronaldo amefunga bao lake la 981 katika ushindi wa mabao 3-1 uliopatikana dhidi ya klabu ya Neftchi Fargona kutoka Uzbekistan, kwenye mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Asia (AFC Champions League Elite).
-
Matokeo ya Mwisho: Al Nassr FC 3-1 Neftchi Fargona
-
Wafungaji wa Al Nassr FC:
-
Angelo (33′)
-
Cristiano Ronaldo (42′)
-
Gofurov – Alyjiumba (78′)
-
-
Wafungaji wa Neftchi Fargona:
-
Odilov (51′)
-
-
Kadi Nyekundu: Alibaev (Neftchi Fargona – 65′)
Ushindi huo unaendelea kuifanya Al Nassr kuzidisha kasi yake kwenye michuano hiyo ya kimataifa, huku macho ya ulimwengu wa soka yakiendelea kumfuatilia Ronaldo katika safari yake ya kuelekea rekodi ya mabao 1,000.
