Waziri Mwigulu: Tusisubiri EL NINO Kama Harusi

Waziri Mwigulu: Tusisubiri EL NINO Kama Harusi
Waziri Mwigulu: Tusisubiri EL NINO Kama Harusi

Waziri Mwigulu: Tusisubiri EL NINO Kama Harusi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Viongozi na Wananchi kuendelea na shughuli za maendeleo licha ya mvua zinazotarajiwa kutokana na El Niño, huku wakichukua tahadhari zinazohitajika.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kongani ya Viwanda ya HWTZ SEZ, Bagamoyo, Mkoani Pwani, Dkt. Mwigulu amesema “mvua ya El Niño isiwe kigezo na sababu, kila shughuli inasimama kisa mvua, muendelee na kazi, siyo tunasubiria kama harusi,”

Aidha, ameiagiza Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na TISEZA, Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Bagamoyo, kuharakisha tathmini na ulipaji wa fidia kwa Wananchi waliopisha eneo la uwekezaji la Zinga lenye ukubwa wa hekta 887, ambao baadhi yao wamesubiri kwa takriban miaka 16.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo amesema Mkoa huo una viwanda 1,768 na Kongani 35 za Viwanda, huku Vijiji vyote 409 vikiwa vimefikiwa na huduma ya umeme.

Mkurugenzi wa HWTZ SEZ, Sophia Su, amesema shughuli za Kampuni hiyo tayari zimezalisha ajira 170, huku idadi hiyo ikitarajiwa kufikia 400 ifikapo Desemba 2026

Related Posts