Haji Manara Awasha Moto: Tatizo la Yanga Siyo Kocha Pekee, Kuna Jingine Zito

Haji Manara Awasha Moto: Tatizo la Yanga Siyo Kocha Pekee, Kuna Jingine Zito
Haji Manara Awasha Moto: Tatizo la Yanga Siyo Kocha Pekee, Kuna Jingine Zito

“Nimeandika weee nimefuta nimeandika tena nimefuta.

Muhimu ndugu zangu tukubali maneno tusiyoyapenda kuhusu team zetu,haijalishi anaesema haumpendi au laa!!

Nichukieni weee Nipendeni weeeee, Usajili wetu ni Mbovu,Hawa foreigners wetu tunaowaleta siku hizi ni Waomba Mungu tu,sitaacha kusema ukweli huu,hadi tusajili Wachezaji kweli sio hawa wa ten naniliu.

Haya twendeni tukamtoe kafara kocha wetu,Kisha tuingie tena sokoni Dirisha dogo”

Ameandika Haji manara mwanachama wa klabu ya Yanga huku akiamini yeye, tatizo la Yanga si kocha pekee hata Usajili wa wachezaji wa Kigeni ulio fanyika dirisha kubwa siyo sahihi.

Haji amewataka viongozi Wa Yanga wasiishie tu kuleta kocha mwingine bali wasajili wachezaji wengine wa Kigeni ambao ni Bora Kuliko hawa waliopo.

Unakubaliana na Haji manara?

Related Posts