
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wamekata tiketi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) kwa msimu wa 2026/27 kufuatia ushindi wa jumla wa mabao 9-1dhidi ya FC 15 De Agosto kwenye hatua ya pili ya awali.
Simba SC wakiwa wageni kikanuni katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam walishinda 6-1 kabla ya kushinda 3-0 dhidi ya FC 15 De Agosto katika uwanja huo huo wakiwa wenyeji na kutinga hatua hiyo.
FT: Simba SC 🇹🇿 3-0 🇬🇶 15 De Agosto (Agg. 9-1)
⚽ 56’ Oura
⚽ 68’ Mpanzu
⚽ 76’ Makgwala
