Kada ya Bavicha Twaha Mwaipaya Adaiwa Kutekwa Nyara Nchini Kenya

Kada ya Bavicha Twaha Mwaipaya Adaiwa Kutekwa Nyara Nchini Kenya
Kada ya Bavicha Twaha Mwaipaya Adaiwa Kutekwa Nyara Nchini Kenya

Hali ya wasiwasi inazidi kutanda mitandaoni kufuatia taarifa za mwanaharakati na kada wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), Twaha Mwaipaya kudaiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana jijini Nairobi, Kenya tukio linalodaiwa kufanyika katika barabara ya Kamulu jijini humo.

Kwa mujibu wa taarifa, watu waliovalia kiraia, waliofunika nyuso zao kwa barakoa wakitumia magari matatu walilizuia gari alilokuwa akisafiria Mwaipaya, wakamshusha kwa nguvu, na kutoweka naye kwenye operesheni inayodhaniwa kupangwa mapema.

Watumiaji wa mitandao na wanachama wa CHADEMA wameeleza wasiwasi wao kuhusu afya na mahali alipo kutokana na mazingira ya kutatanisha ya kutoweka kwake wakitoa wito wa kutaka Mamlaka husika kutoa taarifa za uhakika kuhusu alipo, kulinda usalama wake, na kuheshimu haki zake za kisheria.

Related Posts