Heche Amuomba Rais Ruto Kumhakikishia Usalama wa Twaha Mwaipaya

Heche Amuomba Rais Ruto Kumhakikishia Usalama wa Twaha Mwaipaya
Heche Amuomba Rais Ruto Kumhakikishia Usalama wa Twaha Mwaipaya

Heche Amuomba Rais Ruto Kumhakikishia Usalama wa Twaha Mwaipaya

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amemuomba Rais wa Kenya, William Ruto, kuingilia kati na kuhakikisha mwanaharakati wa Kitanzania na Kiongozi wa Baraza la Vijana wa chama hicho, Twaha Mwaipaya, anapatikana akiwa hai na salama.

Ombi hilo la Heche linakuja kufuatia taarifa zilizosambaa mitandaoni zikidai kuwa Mwaipaya alichukuliwa na watu wasiojulikana Oktoba 25, 2026, katika eneo la Kamulu, Kaunti ya Machakos, karibu na jiji la Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, watu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo walikuwa wakitumia magari matatu, yakiwemo gari aina ya Toyota Land Cruiser Hardtop.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema leo, Heche ameitaka Serikali ya Kenya kushirikiana katika kuhakikisha Mwaipaya anapatikana akiwa salama, huku akieleza wasiwasi wake kuhusu mazingira ya tukio hilo.

“T unajua Serikali ya Kenya haina sababu ya kumteka Twaha, lakini pia tunajua sio rahisi hawa watekaji kuingia nchi nyingine wamchukue mtu bila kusaidiwa na watu wa serikali hiyo. Tunamsihi Rais Ruto na Serikali yake wasaidie kuhakikisha Twaha anapatikana akiwa mzima,” ameandika Heche.

Kauli hiyo inaweka msisitizo katika wito wa kutafutwa kwa Mwaipaya na kuhakikisha usalama wake, huku ikielekeza ombi kwa mamlaka za Kenya kushirikiana katika kufuatilia taarifa hizo.

Hadi wakati wa taarifa hii, madai kuhusu kutekwa kwa Mwaipaya na mazingira ya tukio hilo yanahitaji uthibitisho kutoka kwa mamlaka husika. Hata hivyo, wito wa Heche unaongeza uzito wa juhudi za kutaka kufahamika alipo mwanaharakati huyo na kuhakikisha anapatikana akiwa hai na salama

Related Posts