Tundu Lissu Aanza Rasmi Mgomo wa Kula Gerezani…..

Tundu Lissu Aanza Rasmi Mgomo wa Kula Gerezani.....
Tundu Lissu Aanza Rasmi Mgomo wa Kula Gerezani…..

Tundu Lissu Aanza Rasmi Mgomo wa Kula Gerezani…..

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameanza mgomo wa kula leo, Oktoba 26, 2026, huku chama hicho kikieleza wasiwasi kuhusu kuzuiwa kwa mawakili wake kumwona Gerezani.

Kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA, Mawakili watatu wa Lissu ambao ni Dickson Matata, Doris Kafuku na Neema Massame, walifika Gerezani leo kwa lengo la kukutana na kuwasiliana naye, lakini walizuiwa kuingia.

CHADEMA imesema hali hiyo inazua wasiwasi kuhusu upatikanaji wa msaada wa kisheria kwa Lissu na namna haki zake zinavyolindwa akiwa gerezani, hasa wakati huu ambao ameanza mgomo wa kula.

Chama hicho kimezitaka mamlaka husika kuruhusu mawakili wake kukutana na Lissu bila vikwazo visivyo na msingi wa kisheria, huku kikisisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama na ustawi wake.

CHADEMA imesema inaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya mwenyekiti wake na itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu maendeleo ya suala hilo.

Related Posts