
Boka Anaubonda Mpira Lakini Kuna Sehemu Akifika Anasubiri Kwa Zimbwe
Kwenye maisha, Mungu hakunyimi kila kitu. Huenda akakukosesha kasi kubwa au nguvu za kutosha, lakini akakupa kitu cha thamani zaidi: akili, utulivu na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.
Ukimuangalia Mohamed Hussen kwa sasa, huenda asiwe fullback mwenye kasi kubwa wala nguvu za kupambana kimwili, lakini linapokuja suala la kutumia akili na kufanya maamuzi sahihi, hasa anapofika kwenye eneo la mwisho la mpinzani, jamaa ni zaidi ya mwalimu!
Ameendelea kuonyesha darasani uwanjani namna ambavyo fullback anatakiwa kucheza anapokuwa kwenye eneo la hatari la mpinzani. Anajua wakati wa kupandisha mashambulizi, wakati wa kutoa pasi, namna ya kuchagua eneo sahihi na jinsi ya kufanya maamuzi yanayoisaidia timu.
Huyu ni mchezaji anayethibitisha kwamba soka si suala la kasi na nguvu pekee, bali pia ni mchezo wa akili, utambuzi na kufanya maamuzi kwa wakati sahihi.
Kwangu mimi binafsi, Mohamed Hussen ni miongoni mwa mabeki bora wa pembeni kuwahi kutokea. Si kwa sababu ya kasi yake, bali kwa namna anavyoielewa nafasi yake na kuifanya ionekane rahisi kwa wengine.
Wakati mwingine, kipaji kikubwa si kukimbia kwa kasi zaidi ya wengine, bali ni kujua pa kwenda, wakati wa kwenda na nini cha kufanya unapofika hapo
